Mtu mmoja aliefahamika kwa jina la Wilison Bahati mwenye umri wa miaka 20 mkazi wa kijiji cha Kashelo wilaya ya Mbongwe mkoani Geita amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa madai ya kukosa nauli ya mke wake ili wasafiri kwa ajili ya kwenda kuhudhuria mazishi ya mmoja wa ndugu wa mke kwake.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo afisa mtendaji wa kijiji cha Kashelo wilayani Mbogwe Mkoani Geita Alfred Msekuzi amesema baada ya tukio hilo kutokea alitoa taarifa katika kwa jeshi la polisi wilayani humo na askari walifika na kufanya uchunguzi wa tukio hilo na baadae familia ikaruhusiwa kuendelea na shughuli za mazishi ya ndugu yao.
Akisimulia tukio hilo mke wa marehemu Grace Jeremia amesema mume wake aliamka asubuhi na kumuaga kuwa anakwenda shambani lakini baadaye wakamkuta amejinyonga hali ambayo ilisababisha kupelekea kifo chake.