Zacharia anakwenda jela miaka 30 kwa kumnajisi mwanafunzi

Bakari Zacharia (23) mkazi wa Nyasubi amehukumiwa kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kumnajisi mwanafunzi wa kidato cha pili anayesoma shule ya sekondari Nyasubi mwenye umri wa miaka 15.

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Christina Chovenye, ametoa hukumu hiyo leo na kwamba mtuhumiwa alikuwa Muhudumu wa Baa iitwayo Meru Garden, ambapo alikamatwa Julai 27,,2023 akiwa na mwanafunzi huyo akimuweka kinyumba.

Katika hukumu yake, Hakimu Chovenye amesema Bakari alikutwa na hatia baada ya kuishi na binti huyo kwa kipindi cha mwezi mmoja, ingawa katika utetezi wake alikana kumfahamu binti huyo na kwamba hajawahi kumuona.

Hakimu Chovenye amesema daktari alithibitisha kuingiliwa kimwili mwanafunzi huyo mara kwa mara na mwanafunzi alikiri kuishi kiunyumba na mtuhumiwa na kumuita ni mume wake.

Mwanafunzi huyo katika maelezo yake amesema walikuwa wanafahamiana na kukubaliana waoane na kuanza kuishi wote, ingawa wakati kesi inaendelea binti alifanya jaribio la kujiua kwa kunywa sumu, ambapo ndugu walimuwahi na alitoa ushahidi wake mahakamani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *