Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Asilimia 80 Ya Madereva Wana Matatizo Ya Macho

Imeelezwa kuwa uwepo wa matukio ya ajali za barabarani kwa kiasi kikubwa unachangiwa na matatizo ya macho yanayowakumba baadhi ya madereva kutokana na madereva wengi wa magari kuendesha magari bila kufanyiwa vipimo vya macho.

A tired driver holding his head. Exhausted and tired driver driving a car at sunset.

Hayo yameelezwa na mtaalamu wa matibabu ya uoni hapa nchini ndugu Emmanuel Ezekiel katika maadhimisho ya wiki ya uoni duniani yanaofanyika pale jijini Mwanza ambapo amesema mpaka sasa asilimia 70 mpaka 80 ya madereva waliofanyiwa vipimo vya macho wamebainika kuwa na matatizo ya macho hali ambayo inaweza kuwa chanzo cha ajali barabarani.

Kwa upande wake Eliabu Modest ambaye naye ni mtaalamu wa macho amesema moja ya changamoto ambayo inaweza kumsababishia mtu kuwa na tatizo la uoni hafifu ni matumizi ya pombe kupitiliza, uvutaji wa sigara, huku pia watu wenye changamoto ya presha na kisukari wakiwa katika hatari kubwa za kukumbwa na ugonjwa huo.

Nao baadhi ya madereva waliohudhuria katika vipimo hivyo wamekishukuru chama cha uoni kwa kuratibu vipimo hivyo na wamewaomba madereva wengine waweze kushiriki katika vipimo hivyo ili kupunguza ajali ambazo zingeweza kuepukika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *