Abby Chams akataa kumzungumzia Paula, adai hajui anafanya kazi gani

Staa wa muziki wa Bongo Fleva Abigail Chams maarufu kama Abby Chams leo akijibu maswali ya mashabiki wake kwenye Insta LIVE huku akiesema hamchukii mwanamke mwenzake wala mtu mwingine yoyote.

Chams amesema hayo baada ya kuulizwa swali na shabiki kuwa ‘Jamani unamchukia Pau’ kwa majibu mafupi Abigail Chams amesema ‘Mimi siwezi kumchukia mtu, Siwezi kumchukia Mwanamke mwenzangu, Siwezi kumchukia mtu yoyote aliyeumbwa na Mungu. Ningependa mniulize maswali kuhusu kazi yangu, sababu mimi sioni umuhimu wa kuongelea watu ambao hata hatujui kazi zao ni nini, ila tu kutrend kutokana na kudate Wanaume’ – Abigail Chams.

Miongoni mwa maoni ya wadau wengi inahisiwa kuwa Abigail anatafuta ‘kiki’ ili kusaidia video ya wimbo wake wa Milele iende mjini, Jambo ambalo linaonyesha Marioo alichukizwa nalo na kulijibia kwenye insta stories.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *