
Msanii Omary Mwanga maarufu kama Marioo, kupitia mtandao wa instagram ameandika ujumbe ambao unahisiwa kama dongo baada ya Abby Chams kufanya Instagram LIVE na kumuongelea kimafumbo mpenzi wake Paula ambapo Abby Chams alisema haoni umuhimu wa kuongelea watu ambao hawajui kazi yake, zaidi ni kutrend tu kwa kutoka na Wanaume.
Marioo na Abigail Chams waliwahi kuingia kwenye headlines za Habari za Burudani baada ya kutoka taarifa kuwa Marioo alifuta verse za Abby Chams kwenye wimbo ambao waliufanya kabla na kisha kumuweka Alikiba.
Usiku wa kuamkia Tar 20 2024 Marioo amendika ‘Mtoto wa watu maskini ya Mungu kajituliza zake kimya lakini watu bado wanataka kutaftia kiki hapo hapo, Thats 💯 Bull*** Disrespectful 😏’ – Marioo.