Mkutano wa 16 baraza la mawaziri la kisekta la nishati Afrika Mashariki wahitimishwa jijini Arusha

Mkutano wa 16 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ulioanza tarehe 12 Februari 2024 katika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo jijini Arusha umehitimishwa.


Katika mkutano huo ulioongozwa na Mwenyekiti wake, Shaibu Hassan Kaduara ambaye ni Waziri wa Maji, Nishati na Madini, Zanzibar ulipendekeza kuwepo kwa mkakati wa pamoja wa Jumuiya wa kukabiliana na kuzuia uharibifu wa miundombinu mbalimbali ya nishati ikiwemo ya usambazaji na usafirishaji.


Aidha, Mkutano huo ulitoa mapendekezo kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuongeza kasi na bajeti ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya nishati katika ngazi ya Taifa na Jumuiya itakayoimarisha upatikanaji wa nishati ya kutosha, bei nafuu, endelevu na salama kwa maendeleo ya Jumuiya na watu wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *