
Mwili wa aliyekua Waziri Mkuu, Edward Lowassa umewasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na tayari safari ya kutoka KIA kuelekea Nyumbani kwake Monduli imeanza.
Lowassa anatarajiwa kuzikwa Jumamosi Februari 17 2024 Monduli, Mazishi yatakayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.