Ruvu Shooting ‘Yauona Mwezi’ Yapata Ushindi Wa Kwanza Championship

Klabu ya Ruvu Shooting FC leo imeandikisha ushindi wao wa kwanza msimu huu kwenye ligi ya NBC Championship, kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbuni FC, uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Timu hiyo ilicheza jumla ya mechi 20 bila ushindi ikipata droo nne (4) na kupoteza michezo (15), hivyo kwa ushindi huo inafikisha alama 7 ikiwa ya mwisho kwenye msimamo, ikifunga mabao 10 na kufungwa mabao 42.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *