Mume wa mwanamtandao na mfanyabiashara Zari The Boss Lady , Shakib amethibitisha kuibiwa na vibaka vitu vyake vya thamani kama vile Simu Mbili,Cheni za Thamani na Kiasi cha Pesa nyumbani kwake Kampala, Uganda.

Shakib ametoa taarifa hiyo katika ukurasa wake wa Instagram huku akibainisha kuonyeshwa video jamaa mmoja anayeshukiwa kufanya uhalifu huo.
