Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON inafunguliwa leo 13 Januari 2024 nchini Ivory Coast huku wenyeji wakifungua pazia dhidi ya Guinea Bissau katika uwanja wa Alassane Ouattara mjini Abidjan.
Mkuu wa Shirikisho la Soka barani Afrika CAF, Patrice Motsepe amesema ameridhishwa na hatua za maandalizi zilizofanywa, katika kuepusha maafa yaliyojitokeza nchini Cameroon.
Serikali ya Ivory Coast imewekeza takriban dola bilioni 1.5 katika kuboresha miundombinu katika maandalizi ya mashindano ya mwaka huu. Michuano hiyo inashirikisha timu 24 na itachezwa katika viwanja 6 tofauti kwenye miji mitano.