Mwili wa marehemu Beatrice Minja aliyefariki dunia baada ya kuchomwa visu mara 25 mwilini mwake utazikwa leo kijijini kwao Mbomai Juu Rombo, Kilimanjaro.
Mtuhumiwa wa Mauaji ya Beatrice, Lucas Tarimio alikamatwa Disemba 31,2023 na alifariki dunia Januari 2, 2024 wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro alipokuwa akiendelea kupatiwa matibabu baada ya kunywa sumu ya kuuwa wadudu .
Beatrice alifariki baada ya kukaa hospitali ya KCMC kwa zaidi ya siku 46 katika chumba cha uangalizi maalumu (ICU) na kufariki Disemba 27 2023.