Jumla ya magari 17 ya abiria mkoani Shinyanga yamekutwa na makosa mbalili ikiwemo kusafirisha abiria bila kuwa na leseni ya usafirishaji pamoja na kuzidisha abiria na kutokata tiketi za abiria kwa njia ya mtandao.
Taarifa hiyo imetolewa na Afisa Mfawidhi wa wa Malaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini LATRA , Mkoa wa Shinyanga Denis Magembe wakati wa ukaguzi wa magari uliyofanyika kwa lengo la kubaini wasafirishaji wanaokiuka kanuni na taratibu za usafirishaji wanaokiuka kanuni na taratibu za usafirishaji ambapo kumekuwa na ongezeko la abira na kunachochea uvunjaji wa sheria za usalama barabarani.
Naye Afisa wa LATRA Mkoa wa Shinyanga Julius Kimaro ametumia fursa ya ukaguzi huo kutoa elimu kwa abiria katika mabasi mbalimbali yaliyokamatwa kwenye mchakato huo huku akiwaasa kutambua haki zao ikiwa ni pamoja na kukata tiketi za kusafiria kwa njia ya mtandao .
Baadhi ya wasafishaji kutoka kampuni mbalimbali za usafirishaji wamekiri kuzidisha abiria na kutokukata tiketi za abiria kwa njia ya mtandao wakisema changamoto inayopelekea hali hiyo ni ukosefu wa mtandao kwa baadhi ya maeneo na ongezeko la abiria limekuwa kubwa hivyo inawapelekea kuwahamishia abiria katika magari mengine ambayo hayajapata leseni za usafirishaji ili kuzuia malalamiko kutoka kwa abiria. Mamlaka ya usafiri ardhini (LATRA) imeendesha oparesheni hiyo kwa kushirikiana na jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga kitengo cha usalama barabarani.