.
Staa wa Muziki kutoka Nchini Nigeria Naira Marley ametishia kumshtaki Muigizaji kutoka Nchini humo, Iyabo Ojo kwa madai ya kuwa alimchafua kwa kuchapisha habari za uongo kipindi cha kesi ya aliekuwa msanii wake Marehemu Mohbad.
Naira ameweka wazi kuwa kama muigizaji huyo hataomba radhi kwake basi atamshitaki amlipe Bilioni 1.5 za Kitanzania ambazo ni sawa na Naira Milioni 500.
Barua hiyo ilisema kwamba katika chapisho la Instagram lililochapishwa mnamo Septemba 2023, Iyabo alimshutumu Naira Marley kwa kuhusika na kifo cha marehemu mwimbaji, Ilerioluwa Aloba, maarufu kama Mohbad, kiroho na kimwili.