Jaribio la kumteka mtoto wa Neymar lakwama

Mtu mmoja anashikiliwa na Polisi kufuatia jaribio la kumteka binti wa mshambuliaji wa Brazil, Neymar Jr, siku ya jana Jumanne, Novemba 7, 2023 baada ya kuvamizi nyumbani kwa mpenzi wa Neymar, Bruna Biancardi mjini Sao Paulo, Brazil.

Inaelezwa kuwa wavamizi watatu ambapo wawili kati yao walikuwa na silaha walikuwa wakimsaka Bianciardi na mtoto wake, lakini hawakuwa nyumbani wakati wa uvamizi huo, wala Neymar hakuwepo.

Washukiwa wawili walifanikiwa kukimbia eneo la tukio baada ya kupora mali na vito vya thamani vya Bianciardi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *