Shinyanga kuandaa kongamano la wafanyabiashara

Katika kuhahikikisha maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan juu ya uwepo wa ushirikiano kati ya sekta binafsi na serikali,Mkoa wa Shinyanga unatarajiwa kuandaa kongamano la wafanyabiashara linalotarajiwa kufanyika mwezi Novemba, 2023.

Akizungumza na baadhi ya wawakilishi wa sekta binafsi akiwa ofisini kwake Oktoba 30,2023, mkuu wa mkoa wa Shinganya Mh.Christine Mndeme amesema kuwa kongamano hilo litakalofanyika Novemba 24-26 katika ukumbi wa hoteli ya Karena Manispaa ya Shinyanga litahusisha wafanyabiashara wadogo,wa kati pamoja na wakubwa na wadau wengine wakiwemo wasanii mbalimbali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *