Pogba apigwa stop kucheza soka

Kiungo wa timu ya Juventus, Paul Pogba, mwenye umri wa miaka 30, amesimamishwa kucheza kandanda kwa muda baada ya kukutwa na kosa la kutumia dawa za kusisimua misuli. Uamuzi huo umechukuliwa na Mahakama ya Kitaifa ya Italia yenye dhima ya kupambana na matumizi ya dawa za kuongeza nguvu mwilini.

Aidha, mahakama hiyo imesema Pogba alifanyiwa vipimo baada ya ushindi wa timu yake ya Juventus dhidi ya Udinese kwa mabao 3-0 mnamo Agosti 20, na majibu yalidhihirisha kuwa mchezaji huyo wa Ufaransa, ambaye hakushiriki mechi hiyo, alikuwa na viwango vya juu vya homoni ya “testosterone.”

Pia, iwapo Pogba atapatikana na hatia ya kutumia dawa za kusisimua misuli, anaweza kupigwa marufuku kushiriki kandanda kwa muda wa miaka miwili hadi minne.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *