Baada ya stori za muda mrefu kuwa Asake amemtema Muongozaji wa video zake za muziki kwa muda mrefu, TG Omori. Hatimaye muongozaji huyo anabainisha ni kweli hawafanyi kazi kama zamani ila sio kwa ubaya.
Akizungumza kupitia Podcast ya Zero condition, TG anabinisha “Kila jambo lina mwisho kama ilivyo kupena talaka na wao huwenda imefika mwisho kwani wamefanya video kama12 hivi na wapo fresh tu! Hawana tatizo lolote, na hii ni biashara kila mtu anauhuru wake.”
Video ya ‘Yoga’ inatajwa kuwa chanzo cha wawili kucha kufanya kazi kwani inadaiwa haikupata watu wengi kama zingine.