HAWA NDIO WATEULIWA WAPYA WALIOTEULIWA NA RAIS SAMIA LEO..

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uhamisho wa Wakuu wa Wilaya wawili na uteuzi wa viongozi mbalimbali ambapo Dkt. Vicent Naano Anney amehamishwa kutoka Wilaya ya Bunda kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Maswa.

Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka imeeleza kuwa, Aswege Enock Kaminyoge amehamishwa kutoka Wilaya ya Maswa kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda.

Aidha, CPA Juma Ajuang Kimori ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenziya Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) akichukua nafasi ya Yona Killagane ambaye amemaliza muda wake.

Naye Prof. Edward Gamaya Hoseah ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Benjamin Mkapa akichukua nafasi ya Dkt. Deo Mtasiwa ambaye amemaliza muda wake.

Uteuzi mwingine ni kama inavyoonekana katika kiambata cha kwanza na cha pili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *