Taarifa ya Jeshi la Polisi Nchini, imeeleza kuwa picha mjongeo inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ya Kijana akikamatwa kwa nguvu, ni tukio la ukamataji lililofanywa na Askari Polisi Februari 20, 2025 katika eneo la Maili Moja Kibaha Mkoani Pwani.
Taarifa hiyo iliyotolewa hii leo Februari 22, 2025 na Msemaji wa Jeshi hilo Nchini, DCP David Misime imeeleza kuwa Mtuhumia huyo Rajabu Hassan alikuwa anatafutwa kutokana na tuhuma mbalimbali za kujihusisha na matukio ya uporaji kwa kutumia pikipiki maarufu kama Vishandu.

“Hata wakati anawakimbia Polisi walipojaribu kumkamata na kuwakimbia katika eneo la Mwendapole pikipiki aliyokuwa anandesha ilikuwa haina namba ya usajili, baadaye Polisi walipofanikiwa kumkamata katika eneo la Maili Moja ilikuwa haina namba ya usajili,” amilieleza sehemu ya taarifa ya Misime.
Ameongeza kuwa, wakati wa ukamataji mtuhumiwa huyo alianzisha vurugu licha Askari Polisi kujitambulisha, lakini walifanikiwa kumkamata na kumfikisha Kituo cha Polisi Kibaha, ili kuendelea na taratibu nyingine za kisheria na kudai kuwa Ndugu zake wanazo taarifa zake.
