AFISA MAUZO MAHAKAMANI KWA UHUJUMU UCHUMI

Afisa Mauzo ambaye pia ni Mfanyabiashara wa Mkoani Arusha, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoani humo na kusomewa mashitaka matatu ikiwemo la kutoa risiti zisizo halali za malipo ya zaidi ya Tshs bilion moja.

Malipo hayo yaliisababishia hasara mamlaka ya mapato Nchini (TRA), huku makosa mengine yakiwa ni uhujumu uchumi na utakatishaji fedha wa zaidi ya Tshs million 335.

Mbele ya Hakimu wa Mahakama, Wakili wa Serikali, Yusuf Mlekwa amesema mtuhumiwa huyo akiwa katika maeneo tofauti ya jiji la Arusha akitumia kifaa cha Kieletronic mali ya Taasisi ya Royal Paint alitoa risiti ya malipo ya zaidi ya bilioni 1.

Kosa la pili, Mshtakiwa anadaiwa katika tarehe tofauti jijini Arusha, alifanya kitendo cha makusudi kwa kutoa risiti za uongo na kuisababisha hasara ya bilion zaidi ya 335 TRA.

Aidha, kosa la tatu ni utakatishaji fedha ambapo katika tarehe tofaut alijipatia zaidi ya million 335 ikiwa ni masalia ya uhalifu ya kutoa risiti za uongo.

Mshtakiwa huyo, hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi na upelelezi bado haujakamilika ambapo imeahirishwa hadi Machi 6, 2025.

Meneja wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Mkoa wa Arusha, Deograsius Shuma akiongelea kesi hiyo amesema oparesheni ya kuwasaka wanahujumu wa Mamlaka hiyo inaendelea ili kuhakikisha wale wote wenye tabia kama hiyo wanafikishwa katika vyombo vya sheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *