Watu 270 Wauawa,600 Wajeruhiwa Gaza

Afisa mkuu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu Martin Griffiths amesema matukio ya uharibifu yaliyoshuhudiwa baada ya operesheni ya kijeshi ya Israeli ya kuwaachilia mateka kutoka kambi ya wakimbizi ya Nuseirat Gaza inathibitisha kwamba kila siku vita vinavyoendelea vinazidi kuwa vya kutisha.

Kulingana na wizara ya afya ya Gaza, zaidi ya watu 270 wakiwemo watoto na watu wengine wasio wapiganaji wameuawa wakati wa mapigano makali kati ya vikosi vya Israel na wapiganaji wa Hamas ndani na karibu na kambi ya wakimbizi ya Nuseirat Jumamosi, katikati ya eneo lenye vita huku zaidi ya watu wengine 600 wameripotiwa kujeruhiwa na hospitali zimezidiwa uwezo.

Griffiths ambaye ni mratibu wa Umoja wa Mataifa wa misaada ya kibinadamu na wasuala ya dharura ameyasema hayo katika katika chapisho lake kwenye ukurasa wa mtandao wa X na kuongeza kwamba kambi ya Nuseirat ndio kitovu cha kiwewe cha tetemeko la madhila ambalo raia wa Gaza wanaendelea kuteseka nalo wakishuhudia miili iliyofunikwa chini na ameeleza kwamba hakuna mahali palipo salama ndani ya Gaza.

Aidha Bw. Griffiths amesisitiza kwamba raia wote lazima walindwe. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *