Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

CCM Kirumba boli Litapigwa Hata Usiku

Gideon Gregory,Dodoma

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.  Hamis Mwinjuma amesema kwasasa Wizara ipo katika hatua ya majadiliano na mmiliki wa uwanja wa CCM Kirumba ambapo pamoja na marekebisho mengine, uwanja huo utawekewa taa ili kuwezesha shughuli za michezo kufanyika hata nyakati za usiku.

Naibu Waziri Mwinjuma ameyasema hayo leo Juni 10,2024 Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Ilemela Mhe. Angeline Mabula aliyetaka kujua ni lini Serikali itatekeleza ahadi ya kuweka taa katika Kiwanja cha cha Mpira cha CCM Kirumba uliyopo Jijini Mwanza.

“Uwanja wa CCM Kirumba ni miongoni mwa viwanja vitano ambavyo vimewekwa katika mkakati wa Serikali wa kuvirekebisha ili kukidhi ubora na viwango vya CAF”, amesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *