Kutoka kiwanda cha Afrobeat, Tiwa Savage ameweka wazi tarehe 10, Mei mwaka huu ndio atachia rasmi filamu yake ya Water and Garri.
Tiwa amebainisha kuwa filamu hiyo itaruka kupitia Prime Video na watazamaji zaidi ya 240 duniani kote wataweza kuishuhudia. Filamu hiyo imewakutanisha wakali kutoka Nollywood, ambao ni Jemima Osunde na Mike Afolayan.