Staa wa muziki Kutoka Nigeria, Davido ameamua kuvunja ukimya usiku wa kuamkia leo Aprili 5,2024 kwa kununua ndege yake binafsi kwa kaisi cha Dola Milioni 70 za Marekani.
Davido aliweka taarifa hivyo katika ukurasa wake wa Twitter (X), hata hivyo msanii wa muziki Samklef aliamua kumpongeza baba mzazi wa Davido, Dr. Adedeji Adeleke na kusema aliyenunua ndege na sio Davido.
Hii ni ndege yake ya tatu kumiliki msanii huyo ambayo ni Bombardier Global 7500, hii ni ndege kubwa zaidi katika kampuni ya Bombardier.