Jambo La Leo

Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

2024 tuendelee kudumisha amani, tukemee udini na ukabila

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa watanzania kudumisha amani, umoja na mshikamano wa kitaifa.

Mpango amesema hayo wakati akizungumza na waumini mara baada ya kushiriki Ibada ya Mwaka Mpya katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska Kiwanja cha Ndege Dodoma ambapo Amesema ni muhimu watanzania kuendelea kukemea na kupinga utengano, udini ukabila pamoja na siasa za chuki.

Makamu wa Rais amewataka watumishi wa umma na viongozi wa umma kutimiza wajibu wao ipasavyo wa kuwahudumia wananchi kwa kufanya kazi kwa uadilifu na kutenda haki wakati wote wanapotoa huduma. Amewasihi kufanya kazi kwa hofu ya Mungu na kuachana na tabia za kuwapa kesi wananchi wasiohusika na kesi hizo. Pia amesema ni vema viongozi wa umma wanapotunga sera na sheria kuhakikisha zinakuwa na manufaa kwa wananchi wengi.

Vilevile amewasihi wazazi na walezi kuhakikisha watoto wote wenye umri wa kuanza shule kwa mwaka huu 2024 wanaanza masomo yao na wakati wote kufuatilia maendeleo ya watoto hao shuleni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *