
(1)WASANII WAPYA WATAMBULISHWA
Miongoni mwa matukio ya burudani yaliyotokea mwaka 2023 ni usajili wa wasanii wapya katika lebo za muziki ambapo Januari Nandy Chini ya African Princess alitambulisha msanii wake mpya aitwaye Yammy na aliweza kutoa EP yake iitwayo Three Hearts.
Pia Novemba 16, lebo ya WCB ilimtambulisha msanii mpya aitwaye D Voice na alitoa albamu yake iitwayo Swahiki Kid.
(2)MARIOO KWENYE MAHUSIANO NA PAULA
Miongoni mwa stori kubwa 2023 ni mahusiano ya kimapenzi kati ya Staa wa muziki Marioo na Paula.
Wawili hao wametengeneza vichwa vya habari zaidi kutokana na mahusiano yao lakini pia jinsi wanavyoonyesha kupena sapoti katika kazi zao.
Paula amekuwa kwenye video za muziki za Marioo zaidi ya mbili. Pia Marioo amekuwa akiudhuria matukio ya Paula kama vile uzinduzi wa kipindi chao na uzinduzi wa duka lake.
Kwa sasa Paula anatajwa kuwa na ujauzito wa Marioo.
(3)SHAMSA FORD AFUNGA NDOA NA MUIGIZAJI MWENZAKE
Mwezi Agosti staa wa Filamu Shamsa Ford alifunga ndoa ya pili na muigizaji wa filamu aitwaye Mlilo.
Wawili hao ambao walitajwa kuwa kwenye mahusiano ya siri huku mwanaume huyo akidaiwa kuwa mume wa mtu walifunga ndoa na kwa sasa wamepata mtoto wao wa kwanza na mtoto wao watatu kwa kuwa kila mmoja kabla ya ndoa hii alifanikiwa kupata mtoto.
(4)PROFESA JAY AREJEA KWENYE GAME
Baada ya kupata maradhi kwa muda mrefu, staa mkongwe wa muziki Profesa Jay anarejea tena kwenye game huku akiachia EP yake ya Nusu Pepo nusu Kuzimu ambayo ameshirikisha wasanii kadhaa kutoka hapa nyumbani lakini pia anaanzisha taasisi yake ambayo inaenda kusaidia wale wote wenye matatizo ya Ini
(5)NDOA YA DULLAH MAKABILA KUVUNJIKA, MKE AKIMBIKIA KWA HAJI MANARA
Mwaka huu Dullah Makabila alifunga ndoa na muigizaji aitwaye Zaylisa, ndoa ya wawili hawa ni miongoni mwa ndoa za mastaa wa Bongo zilizodumu muda mfupi.
Dullah na Zaylisa walianza mahusiano kwa kasi na wakafunga ndoa, ila kuanzia mwezi Julai story zikawa kuwa wawili hawa wameachana na ikapelekea mke wa Dullah, Zaylisa kudai alikuwa akipokea vipigo kutoka kwa mume.
Baada ya hapo Zaylisa amekuwa akiwa karibu na Haji Manara na kwa sasa wanatajwa kuwa ni wapenzi na hivi karibuni wanaweza kufunga Ndoa.
Mahusiano ya wawili hawa yamekuwa yakijadiliwa kila siku mitandaoni na hivi karibuni wamesema wanapendana na sio sababu ya pesa wala umaarufu.
(6)RUNGU LA BASATA LIMETEMBEA
BASATA pia mwaka huu hawakuwa mbali na wasanii wake, kwani Waliwafungia wasanii watatu ambao ni Mbosso, BillNas na Whozu na kuwatoza faini ya Mil.3, kwa kosa la kuachia video ya Ameyatimba RMX ikiwa na maudhui mabovu kwa jamaii.
Hata hivyo BASATA iliwasamehe wasanii kwa kwa masharti kadhaa ikiwemo kulipa faini husika na kuifuta ngoma hivyo kwenye mitandao yote na kujirekebisha kwenye maudhui.
Pia hivi karibuni BASATA ilitembeza rungu tena kwa Madee kwa kosa la kuachia wimbo uliokosa maadili na walimtoza faini ya Mil. 3. Bila kuchelewa Madee alifuata masharti ya Baraza na sasa amefunguliwa.
(7)HIP HOP BONGO ILIVYOTISHWA NA KHALIGRAPH JONES
Rapa kutoka Kenya Khalighraph alidiss wasanii wa Bongo kwenye muziki wa Hip Hop na kupelekea wasanii kama Rosa Ree, Songa, Montra na wengine kumjibu rapa huyo.
Hata hivyo Khali anasema alifanya hivyo kuishitua Rap ya Bongo.
(8)RAYVANNY KUINGIA TUZO ZA GRAMMY
Msanii na mmiliki wa Next Level Music, kutajwa kwenye tuzo za Grammy 2024 upande wa Best Latin album kupitia Maluma (Don Juan) ambayo pia S2kizzy amehusika kutengeza hasa ngoma ya Mama Tetema.
Na tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa Febuari 2024.
(9) JAMBO LA JAMBO NI JAMBO SHY TOWN
Miongoni mwa matukio ni Sikukuu Jamukaya, Ugali Festival na Selebretika na Jambo. Haya ni matukio yaliyoacha alama ya vibe kwenye Mkoa wa Shinyanga na yameandaliwa na Jambo Media
Sikukuu Jamukaya ikifanyika Juni na ikikutanishwa wapenda Vibe wa Singeli, Bongo Flava na Hip Hop mitaabya Shy Com kuanzia mchana hadi Usiku
Ugali Festival imefanyika Desemba 16 na ilikuwa ikitoa alama kwa wapishi wa kusonga Ugali Kanda ya Ziwa na maeneo jirani na washindi waliondoka na zawadi nono.
Pua Selebretika hii ni imefanyika karibu na sikukuu ya Chrismass ambapo familia ziliweza kununua bidhaa za Jambo kwa bei nafuu na siku ya mwisho kulikuwa na burudani kutoka kwa sanii kama stamina, Baddest 47 na Young Killer