Jumla ya watuhumiwa 533 wamehukumiwa Kwenda jela kwa kipindi cha mwaka 2023 kwa makosa mbalimbali ikiwemo ubakaji na ulawiti huku matukio ya uhalifu yakitajwa kupungua kwa asilimia 12 katika mkoa wa Arusha.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari leo Januari 15,2024 ambapo amesema jumla ya watuhumiwa 138 wa makosa ya ubakaji walihukumiwa vifungo mbalimbali gerezani ambapo watuhumiwa 86 walihukumiwa vifungo vya Maisha Jela, watuhumiwa 37 walihukumiwa miaka 30 jela na wengine 15 walihukumiwa miaka 20 jela.
Kwa upande wa makosa ya ulawiti jumla ya watuhumiwa 103 walihukumiwa vifungo mbalimbali jela ambapo watuhumiwa 89 walihukumiwa kifungo cha maisha, watuhumiwa 14 walihukumiwa miaka 30.