Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Wazazi na walezi shirikianeni kulinda usalama wa wanafunzi

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Deogratius Ndejembi amewaelekeza wakuu wa shule za msingi nchini kushirikiana na Wazazi, Walezi na Jamii inayozunguka shule zao ili kulinda usalama wa wanafunzi na kuhakikisha wanadumisha mila, desturi na utamaduni za kitanzania kwa kuwafundisha wanafunzi historia ya Tanzania na kudhibiti matendo maovu yasitokee shuleni.

Ndejembi ametoa maelekezo hayo wakati wa akifungua mkutano mkuu wa Tano wa Umoja wa Wakuu wa Shule za Msingi Tanzania (TAPSHA) na kuongeza kuwa wanapaswa kusimamia nidhamu ya Walimu na Wanafunzi Shuleni wakati wote na kuhakikisha ulinzi wa mali za shule unaimarika wakati wote.

Aidha amewaelekeza Makatibu Tawala na Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kusimamia na kukamilisha kwa wakati miradi yote kwenye maeneo yao kwa kuzingatia thamani ya fedha na miongozo iliyotolewa.

Sambamba na hayo amaeongeza kuwa Serikali itaendelea kuajiri walimu na watumishi wa kada zingine mbali mbali nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *