Jarida la Maxim, lilimtaja mwanadada Ashley Graham (36) kutoka Nebraska, pembezoni mwa Nchini Marekani kuwa ndiye mwanamke mwenye mvuto zaidi 2023 (Sexiest Woman 2023).
Ashley Graham ametajwa na jarida hilo manmo mwezi Aprili mwaka huu, amethibitisha uzuri na urembo wa mwanamke sio tu kuwa na mwili mdogo bali hata watu wa miili kama yake wanaweza kuwa na mvuto zaidi na pia anatajwa kuwa mwanamitindo anayepokea kitita kizuri kwenye tasnia ya mitindo Dunia, pia anautajiri wa kiasi cha Dola Milioni 10 za Marekani.