Waumini wa dini ya Kiislamu wamemtaka msanii Harmonize afute mara moja maneno yake aliyoandika kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii akimfananisha Mwenyezi Mungu na Mwanamke.
Kupitia Insta Story yake , Msanii huyo amesema imemchukua miaka 30 kugundua ya kuwa pengine Mungu ni Mwanamke kwa asilimia Kubwa.
Mmoja ya waumini wa Dini ya Kiislamu Sheikh Masoud amemtaka Harmonize kufuta haraka maandishi hayo akisema Mwenyezi Mungu kwa mujibu wa imani ya dini ya Kiislamu ambayo Harmonize ni muumini wa dini hiyo, hafananishwi na chochote.