Watu wawili wakumtwa na nyara za serikali

Jeshi la Polisi Mkoani Simiyu linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kukutwa na nyara za serikali ambazo ni nyama za Wanyama pori aina ya Pundamilia, Swala impala na Digidigi.

Akithibitisha kukamatwa Kwa watuhumiwa hao kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, ACP Maulid Shaba amesema kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa wakiwa na mapaja matatu, vipande viwili vya nyama ya mbavu na kichwa cha Pundamili, kichwa, paja moja, mguu mmoja wa mbele wa Swala impala na vichwa vinne vya Digidigi.

Aidha kaimu kamanda Shaba amesema watuhumiwa hao pia wamekutwa wakiwa na panga moja, kisu kimoja, tochi mbili, honi za pikipiki na betri mbili za sola pasipo kuwa na kibali.

Kaimu Kamanda Shaba amesema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *