Watu Watatu wamefariki baada ya kufukiwa na kifusi wakati wakichimba Madini katika mgodi wa wachimbaji wadogo namba 3 uliopo eneo la Mwakitolyo Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Akizungumza Na Jambo Fm Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Johari Samizi ameyataja majina ya marehemu hao kuwa ni Fadhili Chikando , Kapa Gervas na Mmoja Aliyetambulika kwa Jina Moja la Ezekiel Ambao. wote ni wakazi wa Kata wa Mwakitolyo.

Aidha Samizi ametoa wito kwa watu wote wanaofanya shughuli zao za kiuchumi katika migodi mbalimbali kuendelea kuchukua tahadhari hususani katika kipindi hiki cha mvua ikiwa ni pamoja na kusitisha kwa muda shughuli za kuingia katika mashimo ya dhahabu hadi msimu wa mvua za elnino utakapopita.
Tangu kuanza kwa Msimu wa Mvua za Elnino
tayari zimesababisha madhara mbalimbali hapa nchini ambapo takwimu zilizotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,zinaonyesha mvua hizo zimesababisha kuanguka kwa nyumba 387 na Kaya 564 kukosa makazi huku wana Kaya 3212 wakiathiriwa na mvua hizo na kati ya hao 10 wamejeruhiwa,lakini pia ekari 8972 zenye mazao zimeharibiwa na madhara zaidi yakitokea katika Halmashauri ya wilaya ya Kishapu na Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.