Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

VIDEO:Chatanda na Jokate watema Cheche

Mwenyekiti wa umoja wa wanawake Tanzania (UWT) Marry Chatanda,amefungua mafunzo kwa makatibu wa jumuiya hiyo huku akiwataka kuyatumia kuongeza idadi ya wananchama na wigo wa wapiga kura lengo likiwa ni kuhakikisha wanajiandaa kushinda uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 na uchaguzi mkuu wa 2025 kwa kumpa kura za kutosha rais Samia Suluhu Hassan.

Chatanda ametoa wito huo jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo hayo yaliyowahusisha makatibu wa UWT wilaya,mikoa na viongozi wa jumuiya hiyo Tanzania bara na Zanzibar kwa lengo la kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao.

Naye Katibu mkuu wa UWT Jokate Mwegelo amesema ushirikiano wa kutosha unahitajika miongoni mwa watendaji wa UWT katika kukiwezesha chama kupata ushindi wa uhakika kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 na uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Jokate ametumia wasaa huo kushukuru uongozi wa UWT katika mikoa ya Dar Es salaam, Morogoro, Kilimanjaro, Kigoma, Kagera, Mbeya, Katavi,Geita na ofisi ya UWT Zanzibar kwa michango yao kusaidia wananchi waliokumbwa na maafa katika mji wa Katesh, Wilayani Hanang’ Mkoani Manyara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *