Mkoa wa Geita unakabiliwa na changamoto kubwa ya udumavu kwa watoto walio na umri chini ya miaka 5 hali ambayo inasababisha kwa kiasi kikubwa kushuka kwa wa watoto shuleni kutokana na changamoto hiyo.
Hayo yamebainishwa na mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela wakati akifungua kikao kazi cha lishe kilichofanyika mjini Geita kwa lengo la kubaini sababu za udumavu huo ambapo amesema mkoa wa Geita unashika nafasi ya 5 kitaifa kwa watoto wenye udumavu huku kati ya watoto 100 watoto 34 wanakabiliwa na changamoto ya udumavu.