Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Wanne kizimbani kwa tuhuma za kuua na kuwachoma moto watu wawili

Watu wanne wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza Januari 31, 2024 na kusomewa shtaka la mauaji ya watu wawili katika kesi namba 2536 ya mwaka 2024.

Akisoma shtaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo ,John Jagadi mwendesha mashtaka, mkaguzi wa Polisi Juma Kiparo ameiambia mahakama hiyo kuwa washtakiwa hao kwa pamoja walitenda kosa hilo Januari 11, 2024 huko wilayani Kwimba kwa kumuua Yusuph Mosha (33) mkazi wa Nyamhongoro na Galila Lutobeka (30) Dereva bodaboda na mkazi Nyamhongoro kwa kuwapiga mawe na kuwachoma moto wakiwatuhumu kwa wizi wa kuku kinyume na kifungu namba 196 na 197 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marejeo ya mwaka 2022.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *