Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Wanawake wapate fursa kufikia maendeleo endelevu ya kidigitali

Jamii imetakiwa kuona umuhimu wa kuhakikisha, jitihada zinazotekelezwa na Serikali zinawapa wanawake fursa ya kushiriki kwenye nyanja mbalimbali za maendeleo ili kufikia maendeleo endelevu ya kidigitali.


Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na makundi Maalum  Dkt. Dorothy Gwajima ametoa wito huo wakati wa Mkutano wa pili wa wanawake na Teknolojia wa Tanzania mkoani Dar Es salaam, ambapo  amesema Serikali inayoongozwa na rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, inatambua kuwa, Teknolojia ni chombo muhimu katika kukuza uchumi, ubunifu, na kuboresha maendeleo ya jamii ambapo Tanzania, kama nchi nyingine duniani, inashuhudia mapinduzi ya kidijitali yanayotoa fursa ya Nyanja zote za kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni na inasisitiza kutumia teknolojia na kukuza maendeleo jumuishi.

Amewataka washiriki kutumia kikamilifu fursa ya Mkutano huo katika kujikwamua kiuchumi na kumiliki njia kuu za uchumi kwani ushiriki wa wanawake katika shughuli za kiuchumi kidigitali husaidia kwa sehemu kubwa kuondokana na ukatili wa aina zote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *