Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Niger, Mali na Burkina faso zatangaza kuundwa kwa jeshi la pamoja kupambana na uasi

Wakuu wa majeshi ya Niger, Mali na Burkina Faso, tawala tatu za kijeshi zilizowekwa ndani ya Muungano wa Nchi za Sahel (AES), wametangaza kuundwa kwa kikosi cha pamoja kupambana na makundi ya kijihadi yanayowashambulia.

Mkuu wa majeshi ya Niger Jenerali Moussa Salaou Barmou, katika taarifa kwa vyombo vya habari amesema  Kikosi hicho  cha pamoja cha nchi za AES kitafanya kazi haraka iwezekanavyo ili kutilia maanani changamoto za usalama katika mataifa hayo.

Ouagadougou na Niamey walitangaza Desemba 2, 2023 katika taarifa ya pamoja kwa vyombo vya habari, kwamba wanaondoka katika kundi la G5 Sahel la kupambana na makundi ya wanajihadi, lililoundwa mwaka wa 2014.

Nchi hizo mbili zilijiunga na Mali, ambayo ilijiondoa kutoka kwa kundi hili Mei 2022.

Lilipoundwa mwaka wa 2014, ili kupigana na makundi ya wajihadi katika Sahel, kundi hilo liliundwa na Mali, Burkina Faso, Niger, Mauritania na Chad.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *