WANANCHI SIMIYU WAOMBA KUSOGEZEWA SOKO KARIBU NA MAKAZI YAO

Na Saada Almasi- Simiyu

Wakazi waishio katika mji mdogo wa Sangamwalugesha wilayani Maswa mkoani Simiyu wameiomba serikali kuwatengea eneo la soko ambalo litawaondolea adha ya kutembea mwendo mrefu kutafuta huduma hiyo.

Wakiongea katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa katika kata ya Sangamwalugesha wilayani humo wananchi hao wamesema inawalazimu kufuata huduma hiyo katika majumba ya watu hali ambayo ni hatari wakati soko rasmi lingekuwepo serikali ingepata fursa ya kupata mapato kutokana na ushuru pamoja na wananchi wangejiingizia kipato kupitia biashara.

Mmoja wa wakazi hao Dotto Salum anasema kuwa wakinamama ndio wanaopata tabu zaidi na kulazimika kufika Maswa mjini ambapo ni umbali mrefu kwani bila kufanya hivyo hakuna huduma yoyote wanayoipata

“Zamani kulikuwa na soko ambalo halikuwa rasmi kwa hiyo watu walikuwa wanauza kwa kuibia ibia hivi sasa limekufa na wanaopata tabu zaidi ni akina mama maana wanalazimika kufuata mahitaji Maswa mjini ambako ni mbali maana asipofanya hivyo huduma hapati” amesema Dotto

Diddas Maulid mkazi wa eneo hilo amesema kuwa maeneo mazuri yapo kinachowashangaza ni kutokuwepo na soko rasmi ambali watajumuika wafanyabiashara na wanunuzi kufanya dhughuli zao

“Maeneo kazuri ya kufanya biashara yapo ajabu ni kwamba kwa nini hatuna soko rasmi?serikali hamjui kuwa kuwepo kwa hili soko kutaingiza mapato ya halmashauri?” Amesema Daddas

Jambo FM ikamtafuta mkurugenzi wa halmashauri hiyo Maisha Mtipa ambaye ameahidi kufanyia kazi changamoto hiyo ili wananchi hao waweze kuondokana na adha wanayoipata kwa sasa.

“Suala hili nimelipokea na ninaahidi kulifanyia kazi haraka iwezekanavyo nitazungumzq na watu wa mipango miji ili waliweke hili katika mkakati tuweze kupata soko eneo hilo” amesema Mtipa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *