WAZAZI NA WALEZI ACHENI TABIA YA KUHUSISHA WATOTO KWENYE UGOMVI.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko amewataka wazazi na walezi kuacha tabia ya kuwahusisha watoto katika ugomvi na migogoro yao ili kupunguza mmonyoko wa maadili katika jamii.

Biteko ameyasema hayo hii leo wakati wa maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Familia iliyofanyika kitaifa mkoani Mwanza ambapo amesema wapo baadhi ya wazazi ambao wamekua wakiwahusisha kuwahusisha watoto migogoro yao ya ndoa jambo ambalo wakati mwingine linachochea watoto wa mitaani.

“Haya mambo ya baba au mama kwenda kushtaki kwa watoto matokeo yake na wao wale watoto wanajenga ukuaji wenye chuki ya kutaka kuyasema mambo ya ndani badala ya kuyamaliza nyie watoto wabaki na amani ili hata akikua akiolewa anakuwa balozi mzuri,” amesema Dk Biteko.

 Awali akitoa salamu za Mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amesema  katika kipindi cha mwaka mmoja 2024/2025 walipokea mashauri 3534 huku kati ya hayo 980 yakihusu migogoro ya ndoa.

“Kwa mwaka 2024/2025 kupitia idara yetu ya ustawi wa jamii tulipokea mashauri 3534 yanayohusiana na mambo mbalimbali lakini muhimu zaidi migogoro ya ndoa tuliyopokea ndani ya mwaka huo mmoja ilikuwa 980 hii inaashiria kuwa migogoro ya ndoa ina athari kubwa katika malezi na makuzi ya watoto.

Aidha pia amesema mkoa wa Mwanza tayari umezindua mkakati wa kukabiliana na kutokomeza watoto wa mitaani, ambapo katika mazungumzoa ambayo alifanya na baadhi ya watoto alibaini kuwa wengi wao wametoka majumbani kutokana na sababu za migogoro ya familia.

“Tuliwaita siku moja watoto wa mitaani kama 1000 tukataka kufanya utafiti kwanini wapo mitaani moja kati ya sababu ambayo walikuwa wakiieleza ni migogoro ya familia kwahiyo wakaamua kuingia mitaani,” amesema Mtanda

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *