MKUU WA WILAYA MASWA AWATAKA TARURA KUHAKIKISHA BARABARA INAPITIKA MWAMASHINDIKE.

Kufuatia changamoto ya mawasiliano ya barabara kwa Wananchi wa kijiji cha Mwamashindike kata ya Mwabalatulu wilayani Maswa mkoani Simiyu mkuu wa wilaya hiyo Vincent Naano amemuagiza kaimu meneja wa mamlaka ya barabara vijijini TARURA kuhakikisha anapata suluhisho la muda ili barabara hiyo iweze kupitika

Naano ameyasema hayo alipokuwa kijijini hapo kusikiliza kero za wananchi wake ambao wametoa changamoto hiyo baada ya kuteseka na barabara kwa muda mrefu

Yunis Bukundi mkazi wa kijiji hicho anasema kuwa akina mama na watoto wamekuwa wahanga wakubwa wa kukatika kwa barabara hiyo kwani pale inapojaa maji na kuleta tope hata pikipiki haiwezi kupita.

“Kuna kipindi barabara inajaa tope ni utelezi tu sasa sisi kina mama na watoto kama tumewabeba kupita hapo ni kazi kubwa maana kuna wakati hata pikipiki haiwezi kuvuka hadi mshuke muisukume tena” amesema Yunis.

Naye Leonard Masanja amesema kuwa sasa hivi kutoka kijiji cha Mwakidiga kuja Mwabalatulu inachukua muda mrefu na kuwalazimu kupitia kijiji jirani cha Budekwa muda ambao mtu angefanya kazi nyingine ya kumuingizia kipato

“Ukitaka kuja moja kwa moja kutoka Mwakindiga kuja Mwabalatulu lazima ukwame hapapitiki kwa hiyo tunalazimika kupita kwa njia ya kijiji jirani cha Budekwa ambacho pia muda mrefu sana tunatumia mtu angekuwa amefanya shughuli zake nyingine” amesema Leonard.

Kufuatia malalamiko hayo mkuu wa wilaya hiyo Vincent Naano akataka kujua kutoka kwa kaimi meneja wa TARURA mhandisi Edward Jinay sababu za kushindwa kutengeneza barabara hiyo ambaye alihusisha mito inayopatikana katika barabara hoyo na kuchelewa kwa matengenezo

” tunakiri TARURA tuna taarifa za hii barabara lakini sasa hivi tumeomba tuongezewe fedha maana inahitaji shilingi milioni 700 za ukarabati kwani hii barabara ina mito mingi ambayo imekatiza katikati “amesema mhandisi Edward.

Hata hiyo Naano amekatoa agizo kwa wakala huyo kutafuta suluhisho la muda mfupi litakalo wawezesha wakazi hao kupita kwa urahisi katika barabara hiyo wakiwa wanasubiri suluhisho la kudumu

“kwa sasa tafuteni njia ambayo wakazi hawa watapita kwa urahisi kwa sababu barabara hiyo nimeiona inatakiwa kuwekewa kifusi na imepita katika mashamba ya mpunga sasa lazima utatuzi ufanyike kabla hali haijawa mbaya zaidi” amesema Naano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *