Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila kuwachukulia hatua wote waliohusika na uchomaji wa majengo katika soko la Kariakoo, Dar es Salaam.
Mchengerwa ameyasema hayo leo alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa soko la Kimataifa la Kariakoo, jijini Dar es Salaam.
“Kosa la uchomaji wa majengo ni kosa kubwa sana, na linaweza kupelekea kifungo cha hadi miaka 30,”
“Wale wote waliopelekea moto huu kuzuka, na kusababisha hasara kwa watanzania wakamatwe mara moja na wafikishwe mahakamani.” amesema Waziri Mchengerwa
Aidha, Mkuu wa Mkoa amesema amepokea maagizo hayo na atawachukulia hatua waliofanya uhalifu huo, hata hivyo amesema soko hilo litafungwa CCTV Camera ili kuwabaini wahalifu.