Hii ni Ijumaa ya kwanza ya Mwezi Agosti ambapo Jambo FM tunakupa orodha ya video tano za muziki wa Bongo, ambazo zimeshika nafasi ya juu zadi.

Namba 1: Zuchu – Honey
Video ya ngoma hii ina watazamaji wapatao Milioni 2.3 ndani ya siku saba, na ipo namba 1 on Trending for music.
Namba 2: Alikiba – Mnyama
Hii ni ngoma kwaajili ya klabu ya Simba SC, imetoka siku mbili zilizopita na ina watazamaji laki 628, ipo namba 2 on Trending for music.
Namba 3: Jux Ft Diamond Platnumz – Enjoy
Hii ni audio/sauti na yenyewe inawasikilizaji Milioni 8 na inawiki 2/3 hivi tangu imetoka ipo nafasi ya 3 on Trending for music.
Namba 4: Harmonize – Tena.
Video ya ngoma hii ina siku tatu tangu ilipotoka na ina watazamaji laki 656. Audio imetayarishwa na B BOY BEATS huku ikiwa namba 5 on Trending for music.
Namba 5: Marioo Feat. AliKiba – Love Song.
Hii ni mistari tu ambayo imefanywa kuwa video na imepata kuwa nafasi ya 6 on Trending for music huku ikiwa na watazmaji/wasikilizaji laki 507.