Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Imani Kajula (kushoto) akiwa na Rais wa Klabu ya Yanga, Hersi Said kwenye eneo la wageni wa Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson.
Baada ya kuwatambulisha Dkt. Tulia alitangaza matokeo ya mashindano ya Azania Bunge Bonanza yaliyowashirikisha wabunge wapenzi wa Yanga na Wabunge wapenzi wa Simba na watumishi wa wabunge kwenye viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma Jumamosi Januari 27, 2024. Simba walipata ushindi wa jumla na Yanga waliibamiza Simba katika soka jumla ya mabapo 5-4.