Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

VIDEO: Mkude 45 akamata wanafunzi 45 mnadani

Kufuatia kuendelea kusuasua kuripoti kwa wanafunzi shuleni husani wa madarasa ya awali kwa shule za msingi na kidato cha kwanza kwa shule za sekondari wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Mkuu wa wilaya hiyo Joseph Mkude kwa kushirikiana na jeshi la polisi leo wamefika katika mnada wa Mhunze kwa ajili ya operation ya kuwatafuta watoto wote waliotakiwa kuwa mashuleni baada ya kutembelea shule za sekondari za Isoso na Kishapu na kukuta mahudhurio hafifu kwa wanafunzi waliotakiwa kuripoti kuanza masomo katika shule hizo.

Akizungumza na Jambo FM Mkude amesema wamefanikiwa kuwakusanya wanafunzi 45 waliotakiwa kuripoti katika shule tofauti wilayani humo huku akitoa wito kwa wazazi kuwapeleka watoto hao mashuleni ili waanze masomo kama utaratibu unavyotaka kinyume na hapo sheria itachukua mkondo wake ambapo amehaidi operation hiyo ya kuwasaka wanafunzi katika minada masokoni na majumbani kuwa itakuwa ni endelevu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *