Serikali Mkoani Shinyanga imeanza zoezi la ugawaji wa dawa kwa wananchi kwa ajili ya kutibu maji ya kwenye visima na vyanzo vingine vya maji ikiwa ni pamoja na vyombo vya kuhifadhia maji yakiwemo matanki ili kuua vijidudu na vimelea vinavyosababisha ugonjwa wa kuhara na kutapika.
Kaimu Mganga Mkuu Wa Mkoa Wa Shinyanga Faustine Mulyutu Akizungumza Na Jambo Fm, amesema tayari Wagonjwa 34 Wameruhusiwa Kurudi Nyumbani na wagonjwa Wengine 18 wanaendelea na matibabuna hakuna mgonjwa aliyefariki kutokana na Kipindupindu.