Katunda FC imetwaa ubingwa wa ligi ya taifa Wilaya ya Shinyanga,

Timu ya Katunda FC, yenye maskani yake maeneo ya Katunda Shinyanga, imetwaa ubingwa wa ligi ya taifa wilaya ya Shinyanga, kufuatia ushindi wa mikwaju ya Penati 5-4 dhidi ya Rangers FC, baada ya sare 1-1 ndani ya dakika 90, kwenye fainali iliyopigwa uwanja wa Shy Com.

Huu ni ubingwa wa kwanza kwa Katunda FC ikiwa ni Kwa mara ya kwanza timu hiyo mpya inayoundwa na vijana inashiriki ligi hiyo, huku ikitokea kuwa ‘Best Loser’ hadi kutwaa ubingwa.

Katibu wa chama cha soka Wilaya ya Shinyanga (Shidifa) ambaye pia ni Mratibu mkuu wa Tff mkoa wa Shinyanga Seleman Magubika, ameipongeza timu hiyo na kusema kuwa imetoa somo kubwa kwamba imani kwa vijana wenye vipaji ndio msingi wa kuwawezesha kufikia malengo yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *