Jambo La Leo

Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Uwanja wa Taifa wageuka malisho ya Ng’ombe

Wakazi wa Majengo Halmashauri ya Manispaa ya Kahama wamewaomba wanaosimamia uwanja wa Manispaa ya Kahama maarufu kama Uwanja wa Taifa kuutuza uwanja huo.

Uwanja huo ambao unasimamiwa na Halmashauri ya manspaa ya Kahama umeonekeana kugeuka malisho ya mifugo hasa inapofika wakati wa jioni

Imebainika wafugaji na wachungaji huingiza mifugo yao majira ya saa kumi jioni wakati shughuli nyingi zikiwa zinaendelea.

Wakizungumza na Jambo FM wakazi wa maeneo hayo wamesema uwanja huo ambao unatumika kwa Shughuli za michezo pamoja na shughuli nyingine za kijamii ndiyo uwanja pekee unaotegemewa na wakazi wa Halmashauri hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *