Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Walala Nje, Nyumba zajaa maji.

Wakazi wa mtaa wa Mwatulole kata ya Buhalahala Halmashauri ya Mji wa Geita Wilaya na Mkoa wa Geita wamelazimika kulala nje kutokana na Maji kujaa katika makazi yao yaliyosababishwa na Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Geita hali iliyopelekea maji kuingia hadi ndani kwenye makazi ya watu.

Wakizungumza na Jambo Fm baada ya kufika katika eneo la tukio wamesema  baada ya Mvua iliyonyesha kwa zaidi ya masaa 5 mitaro ya kupitishia maji iliziba kutokana na uchafu kujaa hali iliyopeleka maji kuacha njia na kuingia kwenye makazi yao na kuiomba serikali iwasaidie kutengeneza mitaro.

Wakazi hao wamesema kutokana na Mvua hiyo kuharibu hadi miundombinu ya vyoo katika maeneo hayo, afya zao ziko hatarini kwani hali hiyo inaweza kusababisha magojwa ya mlipuko kutokana na uchafu wa vyoo kusambaa katika makazi ya wananchi.

Diwani wa Kata ya Buhalahala, Doto Zanzui amesema  zaidi ya kaya 30 zimeathirika na mvua hiyo hasa katika eneo la barabara ya Bugomola katika mtaa wa Mwatulole  huku akisema maji hayo yamesababishwa zaidi na ujenzi wa baabara ya Mwatule senta-Lukalanga kwa kiwango cha lami na ujenzi wa barabara hiyo ukikamilika kutamaliza kabisa changamo hiyo.  

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *