Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Urusi yakanusha kuhusika na kifo cha Yevgeny Prigozhin

Msemaji wa Putin Dmitry Peskov aliambia BBC kwamba madai ya Kremlin kutoa amri ya kumuua Yevgeny Prigozhin ni “uongo mtupu”.

Kauli imetolewa wakati wa simu ya mkutano kati ya waandishi wa habari na msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov leo.

Wakati wa simu hiyo, Peskov alimwambia mwandishi wa BBC Will Vernon “kulikuwa na uvumi mwingi” kuhusu ajali ya ndege na “kifo cha kutisha” cha abiria waliokuwemo.

Aliendelea, ‘Huko Magharibi bila shaka uvumi huu unatoka kwa pembe fulani. Yote ni uwongo kabisa. Bila shaka tunapozungumzia suala hili tunapaswa kuongozwa na ukweli tu.

‘Hatuna ukweli mwingi kwa sasa, ukweli unahitaji kufafanuliwa wakati wa uchunguzi rasmi ambao unafanywa sasa’.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *