Wanaomzushia Burna Boy wachanwa

Unaikumbuka ile interview aliyowahi kufanya Burna Boy Machi 2023 na kukaririwa kuwa aliwasema vibaya watu weusi wa Marekani, kuwa hawajui utamaduni wao?? Sasa Burna Boy amefunguka kupitia mahojiano aliyofanya na Complex na kusema kauli yake ilitafsiriwa vibaya tu na watu.


“Watu waliosema hivyo Wamarekani Weusi hawana utamaduni wana ajenda zao. Ukitazama video ya mahojiano, niliyofanya unaweza kunionyesha sehemu ambayo nilisema Wamarekani weusi hawana utamaduni?”, amesema staa huyo

Akaongeza “Hakuna kitu nilichosema ambacho Malcolm X hakusema. Lakini ni wazi, ni Burna Boy anayesema na anatoka Afrika hivyo unaendeza ajenda yako kwa kikundi chako kidogo ili nionekane sifai.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *